-
by
Victor Abuso
Mwishoni mwa juma hili mashabiki wa soka barani Afrika watakuwa katika viwanja mbalimbali kushuhudia michuano ya makundi kufuzu katika fainali za mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.
Afrika Mashariki siku ya Jumamosi, Burundi watakuwa wenyeji wa Niger jijini Bujumbura huku Uganda Cranes wakiwa ugenini kumenyana na Comoros.
Amavubi Stars ya Rwanda itakuwa nyumbani katika uwanja wa Amahoro kukipiga na Black Stars ya Ghana. Huu ni mchuano ambao wadadisi wa soka wameuelezea kuwa utakuwa kama vita kati ya Goliath na Daudi.
Mchuano mwingine unachezwa siku ya Jumamosi ni kati ya Tanzania ambao watakuwa nyumbani katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kumenyana na Super Eagles ya Nigeria.
Mchuano huu ni muhimu kwa makocha wa timu zote mbili ambao wanavinoa vikosi vyao kwa mara ya kwanza katika mashindano haya ya kufuzu.
Kocha wa Tanzania Charles Boniface Mkwasa ataongoza Taifa Stars kutafuta ushindi wake wa kwanza sawa na Sunday Oliseh wa Nigeria.
Tanzania ilikuwa imepiga kambi nchini Uturuki kwa muda wa wiki moja kujiandaa kwa mchuano huu muhimu.
Sudan Kusini pia watachuana na Equatorial Guinea huku Sudan wakiwa ugenini kupambana na Gabon.
Mechi zingine zitakuwa ni kati ya Guinea Bissau dhidi ya Congo Brazaville, Ushelisheli na Ethiopia na Mauritania watawavaa Afrika Kusini nyumbani.
Siku ya Jumapili pia itakuwa ni siku nyingine ya kujitupa viwanjani.
Harambee Stars ya Kenya itakuwa katika uwanja wake wa kihistoria wa Nyayo jijini Nairobi kupambana na mabingwa wa mwaka 2012 Chipolopolo ya Zambia.
Zambia inasema inaiheshimu Kenya na inatarajia mchuano mgumu jijini Nairobi.
Rais wa Shirikisho la soka nchini humo Sam Nyamweya amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono Stars.
Nayo Leopard ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itakuwa ugenini kupambana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo jijini Bangui.
Swaziland watacheza na Malawi, Zimbabwe dhidi ya Guinea huku Chad wakimenyana na Misri jijini Djamena.
Gambia nao wataivaa Cameroon huku Libya wakiwa wenyeji wa Cape verde.
CAF Confederation Cup
Simba snatch late winner against CS Sfaxien as Enyimba beaten
CAF Champions League
Sundown CL campaign has a pulse after beating Raja
Africa Cup of Nations
Zambia end Afcon campaign with comfortable win over Sierra Leone
Africa Cup of Nations
Tanzania,Mozambique,Botswana Qualify for Afcon 2025 in Morocco
Africa Cup of Nations
Zimbabwe Afcon hopes dashed after loss to Cameroon
CAF Champions League
TP Mazembe win CAF Women’s Champions league trophy
CAF Champions League
Mamelodi Sundowns Off to a Lukewarm Start in 2024/25 CAF Champions League
CAF Champions League
AL Ahly start CAF CL campaign with win over Stade d’Abidjan
CAF Confederation Cup
Simba make good start beating Bravos do Maquis
CAF Confederation Cup
Enyimba fall to Al Masry in Alexandria
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...