-
by
Victor Abuso
Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Rwanda Johnathan McKinstry, amekitaja kikosi cha wachezaji 26 kumenyana na Mauritius katika mchuano muhimu wa kundi H kufuzu katika fainali za mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017.
Mchuano huo utapigwa katika uwanja wa Anjalay mjini Belle-Vue, tarehe 26 na baadaye mchuano wa marudiano tarehe 29 katika uwanja wa Amahoro jijini Kigali. Rwanda inakwenda katika mchuano hii ikiwa ya pili kwa alama 3 katika kundi hilo, baada ya kupata ushindi katika mchuano wao dhidi ya Msumbiji wa bao 1 kwa 0 mwaka uliopita na baadaye kufungwa na Ghana bao 1 kwa 0. Kundi hili linaongozwa na Ghana ambayo ina alama 6. Kocha McKinstry, amewateua wachezaji sita katika kikosi chake cha mwisho pamoja na 20 wanaocheza soka nyumbani. McKinstry amesema ni lazima vijana wake, washinde ugenini na nyumbani ili kuendelea kuweka hai matumaini yao ya kufuzu katika fainali ya mwaka 2017 nchini Gabon. Wachezaji walioitwa watakutana siku ya Jumamosi jijini Kigali na kuanza mazoezi ya pamoja kabla ya kuondoka nchini humo siku ya Alhamisi juma lijalo kwenda nchini Mauritius. Kikosi kamili Makipa: Eric Ndayishimiye (Rayon Sports), Olivier Kwizera (APR Fc), Marcel Nzarora (Police Fc) and Andre Mazimpaka (Mukura VS)
Mabeki: Michel Rusheshangoga (APR Fc), Fitina Omborenga (SC Kiyovu), Celestin Ndayishimiye (Mukura VS), Abouba Sibomana (Gor Mahia, Kenya), Soter Kayumba (AS Kigali), Abdul Rwatubyaye (APR Fc), Emery Bayisenge (APR Fc) and Salomon Nirisarike (STVV)
Viungo wa Kati: Yannick Mukunzi (APR Fc), Djihad Bizimana (APR Fc), Jean Baptiste Mugiraneza (Azam Fc, Tanzania), Amran Nshimiyimana (Police Fc), Haruna Niyonzima (Young Africans, Tanzania), Dominique Savio Nshuti (Rayon Sports), Innocent Habyarimana (Police Fc), Jean Claude Iranzi (APR Fc), Yussufu Habimana (Mukura VS) and Muhadjiri Hakizimana (Mukura VS)
Washambuliaji:Ernest Sugira (AS Kigali), Quentin Kwame Rushenguziminega (Laussane Sport, Swiss), Elias Uzamukunda (Le Mans, France) and Dany Usengimana (Police Fc).
CAF Confederation Cup
Simba snatch late winner against CS Sfaxien as Enyimba beaten
CAF Champions League
Sundown CL campaign has a pulse after beating Raja
CAF Champions League
TP Mazembe win CAF Women’s Champions league trophy
CAF Champions League
Mamelodi Sundowns Off to a Lukewarm Start in 2024/25 CAF Champions League
CAF Champions League
AL Ahly start CAF CL campaign with win over Stade d’Abidjan
CAF Confederation Cup
Simba make good start beating Bravos do Maquis
CAF Confederation Cup
Enyimba fall to Al Masry in Alexandria
CAF Confederation Cup
Zamalek got their Group D campaign off to a comfortable star
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...