Na:Victor Abuso
Kocha wa timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji 29 watakaoingia kambini kuanzia Jumapili hii jijini Dar es salaam kwa ajili ya kambi ya wiki moja ya mazoezi.
Mkwasa amewajumuisha wachezaji watano wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi ambao baadaye watajumuika na wenzao katika kambi yao nchini Uturuki.
Taifa Stars inatarajiwa kuweka kambi ya siku 10 jijini Istambul – Uturuki, na itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za Taifa za Libya na Kuwait kabla ya kurejea nchini kumenyana na Super Eagles ya Nigeria mwezi ujao katika mchuano wa kufuzu kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.
Wachezaji watakaongia kambini jumapili ni Makipa: Ally Mustafa (Yanga SC) na Aishi Manula (Azam FC).
Walinzi wa pembeni: Shomari Kapombe (Azam FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Juma Abdul, Mwinyi Haji (Yanga SC) na Abdi Banda (Simba SC).
Walinzi wa kati: Hassan Isihaka (Simba SC), Nadir Haroub, Kelvin Yondani (Yanga SC), Viungo wakabaji: Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam FC).
Viungo washambuliaji ni : Salum Telela (Yanga SC) na Said Ndemla (Simba SC).
Washambuliaji wa pembeni: Orgenes Mollel (Aspire – Senegal), Abdrahman Mbambi (Mafunzo), Deus Kaseke, Saimon Msuva (Yanga SC), Ramdhani Singano, Farid Musa (Azam FC).
Washambuliaji wa kati:John Bocco, Ame Ally (Azam FC) na Rashid Mandawa (Mwadui FC).