Uganda itafungua dimba dhidi ya Ghana katika mchuano wa kwanza wa kundi D, kutafuta ubingwa wa taifa bora barani Afrika katika michuano inayoendelea nchini Gabon.
Mchuano huu unachezwa siku ya Jumanne kuanzia saa moja jioni saa za Afrika Mashariki katika uwanja wa Stade de Port-Gentil.
Ghana ni wazoefu wa michuano hii, lakini Uganda wanarejea katika michuano hii baada ya miaka 39.
Mataifa haya, yanakutana tena baada ya kufanya hivyo mwaka 1978 wakati walipokutana katika fainali ya michuano hii jijini Accra na Ghana kushinda fainali hiyo kwa mabao 2-0.
Kati ya mechi tatu ambazo mataifa haya yamekutana hivi karibuni, Uganda wameshinda Ghana mara moja na kutoka nao sare mara mbili.
Ghana inatafuta taji hili, kwa mara ya kwanza baada ya kushinda taji hili mara ya mwisho 1982.
Black Stars iliwahi kushinda taji hilo pia mwaka 1963, 1965 na 1978.
Mwaka 2015, ilifika fainali lakini ikafungwa na Ivory Coast.
Ratiba nyingine ya kundi D
Misri vs Mali-Kuanzia saa nne usiku saa za Afrika Mashariki.