KUNDI A.
Kundi A lina jumla ya timu nne, wamo wenyeji wa michuano ya mwaka huu, timu ya taifa ya Gabon, Guinea-Bissau, Cameroon na Burkina Faso.
Timu ya taifa ya Gabon:
Timu ya taifa ya Gabon inashiriki michuano ya mwaka huu kama nchi mwenyeji. Timu hii imeshawahi kushiriki mara 6 kwenye michuano hii, na mwaka huu itakuwa ni mara yake ya .
Kwa mara ya kwanza Gabon ilishiriki michuano hii mwaka 1994 na kuishia kwenye hatua ya makundi.
Lakini mwaka 1996 baada ya kufanya vibaya mwaka 94, Gabon ilifika katika hatua ya robo fainali, mafanikio ambayo yalijirudia katika michuano ya mwaka 2012 ambapo ilikuwa nchi mwenyeji na Equatorial Guinea na kufika katika hatua ya robo fainali.
Jina la Utani la timu hii ni “Panthers”, kocha mkuu wa timu hii ni Jose Antonio Camacho.
Kikosi kamili cha Gabon: Kwenye mabano ni timu wanazochezea.
Makipa:
Anthony Mfa Mezui (clubless), Yves Stephane Bitseki Moto (Mounana), Didier Ovono (Ostend/BEL)
Mabeki:
Aaron Appindangoye (Laval/FRA), Bruno Ecuele Manga (Cardiff City/WAL), Franck Perrin Obambou (Stade Mandji), Johann Serge Obiang (Troyes/FRA), Benjamin Ze Ondo (Mosta/MAL), Lloyd Palun (Red Star/FRA), Andre Biyogho Poko (Karabukspor/TUR), Yoann Wachter (Sedan/FRA)
Viungo:
Guelor Kanga Kaku (Red Star/SRB), Mario Lemina (Juventus/ITA), Levy Clement Madinda (Nastic Tarragona/ESP), Didier Ndong (Sunderland/ENG), Junior Serge Martinsson Ngouali (Brommapojkarna/SWE), Merlin Tandjigora (Meixian Hakka/CHN), Samson Mbingui (Raja Casablanca/MAR)
Washambuliaji:
Serge Kevyn Aboue Angoue (Uniao Leiria/POR), Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund/GER, capt), Cedric Ondo Biyoghe (Mounana), Denis Athanase Bouanga (Tours/FRA), Malick Evouna (Tianjin Teda/CHN)
Nahodha wa kikosi hiki ni, Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund/GER).
Timu ya Taifa ya Guinea-Bissau:
Hii ni mara ya kwanza kwa timu ya taifa ya Guinea-Bissau, kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika. Wakati wa mechi za kufuzu, Guinea-Bissau ilimaliza ya kwanza kwenye kundi lake kwa kuwa na alama 10.
Kama ilivyofanya katika hatua ya makundi kufuzu kucheza fainali za mwaka huu, ndivyo ambavyo wadadisi wa soka wanaona kuwa huenda timu hii ikatengeneza historia kwenye michuano ya mwaka huu na pengine kuvuka hatua ya makundi.
Kikosi cha Guinea-Bissau, kinaongozwa na kocha, Bassirou CANDE.
Jina la utani la timu hii ni “Djurtus”
Kikosi Kamili cha timu ya taifa ya Guinea-Bissau: Kwenye mabano ni timu wanazochezea.
Makipa: Papa Mbaye (Orellana/ESP), Jonas Mendes (Salgueiros/POR), Edouard Mendy (Reims/FRA)
Mabeki:
Mama Balde (Sporting Lisbon B/POR), Mamadu Cande (Tondela/POR), Eliseu Cassama (Rio Ave/POR), Eridson (Freamunde/POR), Emmanuel Mendy (Ceahlaul Piatra Neamt/ROU), Formose Mendy (Red Star/FRA), Rudinilson Silva (Lechia Gdansk/POL), Agostinho Soares (Sporting Covilha/POR), Juary Soares (Mafra/POR)
Viungo:
Toni Silva, Zezinho (both Levadiakos/GRE), Abudu (Operario/POR), Aldair (Olhanense/POR), Bocundji Ca (Paris FC/FRA, capt), Abel Camara (Belenenses/POR), Idrissa Camara (Avellino/ITA), Francisco Junior (Stromsgodset/NOR), Frederic Mendy (Ulsan Hyundai/KOR), Jean-Paul Mendy (Quevilly-Rouen/FRA), Pele (Benfica B/POR), Piqueti (Sporting Braga B/POR), Leocísio Sami (Akhisar Belediyespor/TUR), Naní Soares (Gil Vicente/POR), Yazalde (Rio Ave/POR), Ze Turbo (Tondela/POR).
Washambuliaji:
Guti Almada (Real Queluz/POR), Edelino Ie (Sporting Braga B/POR), Joao Mario (Chaves/POR), Mesca (AEL Limassol/CYP), Bruno Preira (Colomiers/FRA), Sana (Academico Viseu/POR)
Nahodha wa timu hii ni, Bocundji Ca (Paris FC/FRA)
Timu ya taifa ya Cameroon:
Timu ya taifa ya Cameroon, imeshawahi kushiriki michuano hii mara 17, na michuano ya mwaka huu itakuwa ni mara yake ya 18 kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika.
Kwa mara ya kwanza timu hii ilishiriki kombe hili mwaka 1970 na kuishia hatua ya makundi.
Cameroon imewahi kutwaa taji la Afrika mara nne (4), mwaka 1984, 1988, 2000 na 2002. Iliwahi kushika nafasi ya pili mara mbili, mwaka 1986 na mwaka 2008. Imewahi pia kufika katika hatua ya nusu fainali mara moja nayo ilikuwa ni mwaka 1992.
Cameroon ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi M ikiwa na alama 14. Jina la utani la timu hii ni “Indomitable Lions” ikiwa na maana ya Simba wasiofugika.
Kocha mkuu wa timu hii ni Mbelgiji, BROOS Hugo
Kikosi kamili cha Cameroon: Kwenye mabano ni timu wanazochezea.
Makipa:
Guy-Roland Ndy Assembe (Nancy/FRA), Jules Goda (Ajaccio/FRA), Georges Mbokwe (Coton Sport), Andre Onana (Ajax Amsterdam/NED), Fabrice Ondoa (Sevilla/ESP)
Mabeki:
Henri Bedimo (Marseille/FRA), Aurelien Chedjou (Galatasaray/TUR), Fai Collins (Standard Liege/BEL), Mohamed Djeitei (Nastic Tarragone/ESP), Ernest Mabouka (Zilina/SVK), Joel Matip (Liverpool/ENG), Michael Ngadeu Ngadjui (Slavia Prague/CZE), Jonathan Ngwem (Progresso Sambizanga/ANG), Nicolas Nkoulou (Lyon/FRA), Allan Nyom (West Bromwich Albion/ENG), Ambroise Oyongo (Impact Montreal/CAN), Maxime Poundje (Bordeaux/FRA), Adolphe Teikeu (Sochaux/FRA)
Viungo:
Ibrahim Amadou (Lille/FRA), Franck Zambo Anguissa (Marseille/FRA), Franck Boya (Apejes Academy), Arnaud Djoum (Hearts/SCO), Franck Kom (Karlsruhe/GER), Georges Mandjeck (Metz/FRA), Sebastien Siani (Ostend/BEL)
Washambuliaji:
Anatole Abang (New York Red Bulls/USA), Vincent Aboubakar (Besiktas/TUR), Christian Bassogog (Aalborg/DEN), Eric-Maxim Choupo-Moting (Schalke/GER), Benjamin Moukandjo (Lorient/FRA), Clinton Njie (Marseille/FRA), Edgar Salli (Saint-Gall/SUI), Robert Ndip Tambe (Spartak Trnava/SVK), Karl Toko-Ekambi (Angers/FRA), Jacques Zoua (Kaiserslautern/GER)
Timu ya Taifa ya Burkina Faso:
Hii ni mara ya kumi (10) kwa timu ya taifa ya Burkina Faso kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika, mara ya kwanza kwa Burkina Faso kushiriki michuano hii ilikuwa ni mwaka 1970.
Mwaka 1998 Burkina Faso kwa mara ya kwanza ilimaliza kwenye nafasi za juu wakati walipoandaa fainali hizi na kumaliza katika nafasi ya nne. Lakini nafasi ya kipekee na mafanikio makubwa iliyowahi kupata timu hii ni mwaka 2013 ambapo ilifika kwenye hatua ya fainali.
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Burkina Faso ni Paulo Duarte, raia wa Ureno. Jina la utani la timu hii ni “Les Étalons” Ikiwa na maana ya Farasi.
Kikosi kamili cha Burkina Faso: Kwenye mabano ni timu wanazochezea.
Makipa:
Herve Koffi (ASEC/CIV), Moussa Germain Sanou (Beauvais/FRA), Aboubacar Sawadogo (Kadiogo)
Mabeki:
Ernest Congo (Khemisset/MAR), Yacouba Coulibaly (Bobo), Issoufou Dayo (Berkane/MAR), Bakary Kone (Malaga/ESP), Souleymane Kouanda (ASEC/CIV), Issoumaila Lengani (Happoel Ashkelon/ISR), Patrick Malo (Smouha/EGY), Issouf Paro (Santos/RSA), Steeve Yago (Toulouse/FRA)
Viungo:
Cyrille Bayala (Sheriff Tiraspol/MDA), Adama Guira (Lens/FRA), Charles Kabore (Krasnodar/RUS, capt), Prejuce Nacoulma (Kayserispor/TUR), Bakary Sare (Moreirense/POR), Blati Toure (Omonia Nicosia/CYP), Abdoul Razack Traore (Karabuspor/TUR), Alain Traore (Kayserispor/TUR), Bertrand Traore (Ajax Amsterdam/NED), Jonathan Zongo (Almeiria/ESP)
Washambuliaji:
Aristide Bance (ASEC/CIV), Banou Diawara (Smouha/EGY), Jonathan Pitroipa (Al Nasr/UAE)
KUNDI B:
Kundi B nalo lina jumla ya timu nne, ambapo kuna timu ya taifa ya Senegal, Algeria, Tunisia na Zimbabwe.
Timu ya Taifa ya Senegal:
Timu ya taifa ya Senegal, imeshiriki michuano hii mara kumi na tatu (13) na katika michuano ya mwaka huu itakuwa ni mara yake ya kumi na nne (14). Mwaka 2002 timu hii ilifanikiwa kucheza hatua ya fainali lakini haikufanikiwa kutwaa taji hili. Mwaka 1990 na mwaka 2006 timu ya taifa ya Senegal ilifanikiwa kufika kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hii.
Senegal ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi K. Kwa mara ya kwanza timu hii ilifuzu kucheza michuano ya Afrika mwaka 1965.
Kocha mkuu wa kikosi hiki ni mzawa, Cisse Aliou. Jina la utani la timu hii ni “Teranga Lions” ikiwa na maana ya Simba wa Teranga.
Kikosi kamili cha Senegal: Kwenye mabano ni timu wanazochezea.
Makipa:
Abdoulaye Diallo (Caykur Rizespor/TUR), Khadim N’Diaye (Horoya/GUI), Pape Seydou N’Diaye (Niarry Tally)
Mabeki:
Saliou Ciss (Valenciennes/FRA), Lamine Gassama (Alanyaspor/TUR), Kalidou Koulibaly (Napoli/ITA), Cheikh M’Bengue (Saint-Etienne/FRA), Kara Mbodj (Anderlecht/BEL), Zargo Toure (Lorient/FRA)
Viungo:
Mohamed Diame (Newcastle/ENG), Papakouli Diop (Espanyol/ESP), Idrissa Gueye (Everton/ENG), Cheikhou Kouyate (West Ham/ENG, capt), Papa Alioune Ndiaye (Osmanlispor/TUR), Cheikh N’Doye (Angers/FRA), Henri Saivet (Saint-Etienne/FRA)
Washambuliaji:
Keita Balde (Lazio/ITA), Famara Diedhiou (Angers/FRA), Mame Biram Diouf (Stoke/ENG), Moussa Konate (Sion/SUI), Sadio Mane (Liverpool/ENG), Ismaila Sarr (Metz/FRA), Moussa Sow (Fenerbahce/TUR)
Timu ya Taifa ya Algeria:
Timu ya taifa ya Algeria imeshiriki michuano hii mikubwa barani Afrika kwa mara 16 na michuano ya mwaka huu inakuwa ni mara yake ya 17, na mara ya kwanza kushiriki michuani hii ilikuwa ni mwaka 1968.
Mafanikio makubwa ambayo Algeria imeyapata toka ilipoanza kushiriki michuano hii, ni kufanikiwa kutwaa taji hili mwaka 1990, ikamaliza kwenye nafasi ya tatu katika michuano ya mwaka 1984 na 1988, ikafika hatua ya nusu fainali katika michuano ya mwaka 1982 na 2010.
Algeria ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi J kwa alama 16. Jina la utani la timu hii ni “Les Fennecs”.
Kocha mkuu wa kikosi cha Algeria ni Mbelgiji, George Leekens.
Kikosi kamili cha Algeria: Kwenye mabano ni timu wanazochezea.
Makipa:
Malik Asselah (JS Kabylie), Rais M’Bolhi (Antalyaspor/TUR), Chemseddine Rahmani (Mouloudia Bejaia)
Mabeki:
Mohamed Benyahia, Mohamed Meftah (both USM Alger),Hichem Belkaroui (Esperance/TUN), Mokhtar Belkhiter (Club Africain/TUN), Ramy Bensebaini (Rennes/FRA), Liassine Cadamuro (Servette/SUI), Faouzi Ghoulam (Napoli/ITA), Aissa Mandi (Real Betis/ESP), Djamel Mesbah (Crotone/ITA)
Viungo:
Mehdi Abeid (Dijon/FRA), Nabil Bentaleb (Schalke/GER), Yacine Brahimi (Porto/POR), Rachid Ghezzal (Lyon/FRA), Adlene Guedioura (Watford/ENG), Riyad Mahrez (Leicester City/ENG), Saphir Taider (Bologna/ITA)
Washambuliaji:
Baghdad Bounedjah (Al Sadd/QAT), Sofiane Hanni (Anderlecht/BEL), Islam Slimani (Leicester/ENG), El Arabi Hillel Soudani (Dinamo Zagreb/CRO)
Timu ya Taifa ya Tunisia:
Timu ya taifa ya Tunisia imeshiriki michuano hii ya kombe la mataifa ya Afrika mara 16, na michuano ya mwaka huu itakuwa ni mara yake ya 17.
Mwaka 1965 Tunisia ilimaliza katika nafasi ya 2 baada ya kufika fainali, sawa na mwaka 1996, lakini mwaka 2004 Tunisia ilifanikiwa kutwaa taji hili la Afrika.
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tunisia ni Mpoland, Henryk Kasperczak. Jina la utani la timu hii ni “Les Aigles de Carthage”.
Kikosi kamili cha timu ya Tunisia: Kwenye mabano ni timu wanazochezea.
Makipa:
Moez Ben Cherifia (Esperance), Rami Jeridi (Sfaxien), Aymen Mathlouthi (Etoile Sahel, capt), Farouk Ben Mustapha (Club Africain)
Mabeki:
Ghazi Abderrazak, Zied Boughattas, Hamdi Nagguez (all Etoile Sahel), Chamseddine Dhaouadi, Ali Machani, Iheb Mbarki (all Esperance), Oussama Haddadi, Bilel Ifa (both Club Africain), Aymen Abdennour (Valencia/ESP), Slimen Kchok (CA Bizertin), Ali Maaloul (Al-Ahly/EGY), Hamza Mathlouthi (Sfaxien), Mohamed Ali Yaakoubi (Caykur Rizespor/TUR), Syam Ben Youssef (Caen/FRA)
Viungo:
Mohamed Amine Ben Amor, Hamza Lahmar, Iheb Msakni (all Etoile Sahel), Saad Bguir, Ferjani Sassi (both Esperance), Larry Azouni (Nimes/FRA), Anis Ben Hatira (Darmstadt/GER), Wahbi Khazri (Sunderland/ENG), Issam Ben Khemis (Lorient/FRA), Yassine Meriah (Sfaxien), Youssef Msakni (Lekhwiya/QAT), Abdelkader Oueslati (Club Africain), Naim Sliti (Lille/FRA)
Washambuliaji:
Ahmed Akaichi (Ittihad Jeddah/KSA), Khaled Ayari (Paris FC/FRA), Nejmeddin Daghfous (Wurzburg/GER), Hamdi Harbaoui (Anderlecht/BEL), Issam Jebali (Elfsborg/SWE), Saber Khalifa (Club Africain), Ahmed Khalil (Al Ahly/UAE), Taha Yassine Khenissi (Esperance), Idriss Mhirsi (Red Star/FRA), Yoann Touzghar (Auxerre/FRA).
Nahodha wa kikosi hiki ni Yassine Chikhaoui.
Timu ya Taifa ya Zimbabwe:
Timu ya taifa ya Zimbabwe imewahi kushiriki michuano hii mara mbili (2), na michuano ya mwaka huu itakuwa ni mara yake ya tatu (3) kushiriki.
Kwa mara ya kwanza Zimbabawe ilifuzu kwenye michuano hii mwaka 2004, na toka wakati huo haijawahi kupata mafanikio makubwa kwenye michuano hii, zaidi ya kuishia katika hatua ya makundi ya michuano hii mikubwa barani Afrika.
Zimbabwe ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi L ikiwa na alama 11. Jina la utani la timu hii ni “Warriors” ikiwa na maana ya mashujaa.
Kocha mkuu wa timu hii ni mzawa, Pasuwa Calistus. Nahodha wa timu ya taifa ya Zimbabwe ni Willard Katsande.
Kikosi kamili cha timu ya taifa ya Zimbabawe: Kwenye mabani ni timu wanazochezea.
Makipa:
Donovan Bernard (How Mine), Nelson Chadya (Ngezi Platinum), Takabva Mawaya (Hwange), Tatenda Mkuruva (Dynamos)
Mabeki:
Teenage Hadebe, Lawrence Mhlanga (both Chicken Inn), Onismor Bhasera (SuperSport Utd/RSA), Liberty Chakoroma (Ngezi Platinum), Bruce Kangwa (Azam/TAN), Oscar Machapa (V Club/COD), Blessing Moyo (Maritzburg Utd/RSA), Elisha Muroiwa (Dynamos), Tendai Ndlovu (Highlanders), Costa Nhamoinesu (Sparta Prague/CZE), Hardlife Zvirekwi (CAPS Utd)
Viungo:
Kudakwashe Mahachi, Danny Phiri (both Golden Arrows/RSA), Khama Billiat (Mamelodi Sundowns/RSA), Talent Chawapiwa (ZPC Kariba), Ronald Chitiyo (Harare City), Willard Katsande (Kaizer Chiefs/RSA, capt), Raphael Kutinyu (Chicken Inn), Marshall Mudehwe (FC Platinum), Marvelous Nakamba (Vitesse Arnhem/NED)
Washambuliaji:
Tinotenda Kadewere (Djurgardens/SWE), Cuthbert Malajila (Wits/RSA), Nyasha Mushekwi (Dalian Yifang/CHN), Knowledge Musona (Ostend/BEL), Tendai Ndoro (Orlando Pirates/RSA), Evans Rusike (Maritzburg/RSA), Mathew Rusike (Helsingborgs/SWE)