Guinea-Bissau iliishangaza Zambia baada ya kuifunga mabao 2-1 jijini Bissau na kujipa matumaini ya kufuzu kucheza fainali ya bara la Afrika kwa mara ya pili.
Zambia, ilianza vema kupitia bao la mchezaji wake Justin Shonga aliyefunga mkwaju wa Free Kick, lakini muda fupi baada ya kuanza kipindi cha pili, Stoppila Sunzu alijifunga na hivyo kuisawazishia Guinea-Bissau huku Toni Silva akiipa timu yake ushindi kwa bao la kichwa.
Kwa matokeo haya Guinea Bissau iangopza kundi lao kwa alama saba, baada ya mechi nne, huku Namibia, Msumbiji na Zmabia zote zikiwa na alama nne.
Jijini Nairobi, Harambee Stars ya Kenya nayo ilipata matumaini ya kurejea katika fainali hizo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 14 baada ya kuifunga Ethiopia mabao 3-0 katika uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani.
Mabao ya Harambee Stars yalitiwa kimyani na Michael Olunga , Eric Johanna na nahodha Victor Wanyama kupitia mkwaju wa penalti. Iwapo Shirikishi la soka duniani FIFA, litaendelea kuifungia Sierra Leon.
Michuano hii inaendelea kesho:-
Tanzania vs Cape Verde Island
Zimbabwe vs Congo DRC
Rwanda vs Guinea
Sudan Kusini vs Gabon
Sudan vs Senegal
Burundi vs Mali
Lesotho vs Uganda