Timu za taifa za mchezo wa soka za Nigeria, Namibia, Guinea-Bissau, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Malawi, zimeanza kwa ushindi, michuano ya kwanza, hatua ya makundi, kufuzu katika fainali ya mwaka 2021, kutafuta ubingwa wa Afrika nchini Cameroon.
Wenyeji Cameroon hawakufungana na wageni Cape Verde, huku Lesotho wakilazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Sierra Leone, jijini Freetown.
Nigeria nao wakicheza nyumbani mjini Uyo, walitoka nyuma na kuwashinda jirani zao Benin mabao 2-1 katika mechi ya kundi L.
Jamhuri ya Kati nayo, iliifunga Burundi mabao 2-0 katika mechi ya kundi E.
Matokeo mengine:
.Namibia 2-1 Chad (Kundi A)
- Malawi 1-0 South Sudan (Kundi B)
- Burkina Faso 0-0 Uganda (Kundi B)
- Sudan 4-0 Sao Tome and Principe (Kundi C)
- Angola 1-3 The Gambia (Kundi D)
- CAR 2-0 Burundi (Kundi E)
- Cameroon 0-0 Cape Verde (Kundi F)
- Guinea Bissau 3-0 Eswatini (Kundi I)
- Senegal 2-0 Congo (Kundi I)
- Nigeria 2-1 Benin (Kundi L)
- Sierra Leone 1-1 Lesotho (Kundi L)
Ratiba ya Alhamisi Novemba 14 2019:
Msumbuji vs Rwanda
Misri vs Kenya
Togo vs Comoros
Mali vs Guinea
Ghana vs Afrika Kusini
DRC vs Gabon
Algeria vs Zambia