Safari ya mataifa ya Afrika kufuzu katika michuano ya Afrika mwaka 2017 yatakayofanyika nchini Gabon, inaanza Jumatano hii.
Hii ni michuano ya makundi kati ya mataifa mbalimbali na michuano ya marudiano itachezwa wiki ijayo.
Harambee Stars ya Kenya tayari imewasili jijini Bissau kumenyana na Guinea Bissau siku ya Jumatano.
Mchuano mwingine wa kundi hili ni kati ya Zambia ambao watakuwa nyumbani kumenyana na Congo Brazavile.
Congo na Zambia zote zina alama nne katika kundi hili, huku Guinea Bissau na Kenya ikiwa na alama 1.
Taifa Stars ya Tanzania nayo ipo jijini N’Djamena kuchuana na Chad katika mchuano muhimu wa kundi G.
Tanzania ina alama 1 katika kundi hili na inaorodheshwa ya tatu nyuma ya Nigeria ambayo ina alama 4, huku Misri ikiwa inaongoza kwa alama 6.
Misri na Nigeria nazo zitachuana siku ya Ijumaa.
Sudan Kusini ambayo imewashangaza wengi katika safari hii kwa kuwa ya pili katika kundi lake la C kwa alama 3 mbele ya Mali ambayo ina alama 4, itakuwa wenyeji wa Benin ambayo ni ya tatu kwa alama 2, huku Equitorial Guinea ikiwa ya mwisho kwa alama 1.
Mechi nyingine siku ya Jumatano ni kati ya Sao Tome e’ Principe dhidi ya Libya.
Siku ya Alhamisi.
Madagascar vs Central Africa Republican
Comoros vs Bostwana
Djibouti vs Liberia
Ghana vs Mozambique
Siku ya Ijumaa
Swaziland vs Zimbabwe
Gabon vs Sierra Leon
Nigeria vs Egypt
Mauritania vs Gambia
Cote d’ivoire vs Sudan
Guinea vs Malawi
Tunisia vs Togo
Mali vs Equatorail Guinea
Algeria vs Ethiopia
Siku ya Jumamosi
Mauritius vs Rwanda
Seychelles vs Lesotho
Burundi vs Namibia
Congo DRC vs Angola
Cameroon vs South Africa
Cape Verde Islands vs Morocco
Burkina Faso vs Uganda
Senegal vs Niger
Siku ya Jumapili.
Mozambique vs Ghana
Kenya vs Guinea Bissau
Bostwana vs Comoros
Congo vs Zambia
Benin vs South Sudan.