Timu ya taifa ya soka ya Afrika Kusini, Bafana Bafana imefuzu katika fainali ya michuano ya kuwania taji la Kusini mwa Afrika COSAFA baada ya kuishinda Swaziland mabao 5 kwa 1 katika mchuano wa nusu fainali uliochezwa siku ya Jumatano usiku nchini Namibia.
Vijana wa kocha Shakes Mashaba, walianza kupata bao katika dakika 9 kipindi cha kwanza kupitia mchezaji wake Aubrey Modiba, huku Reyaad Pieterse akifunga la pili katika dakika ya 18 huku mabao mengine yakipatikana katika kipindi cha pili.
Mwaka uliopita wakati wa michuano hii, Afrika Kusini iliondolewa katika michuano hii katika hatua ya robo fainali.
Vikosi vya timu zote.
Afrika Kusini: Reyaad Pieterse; Tebogo Moerane, Themba Sikhakhane, Rivaldo Coetzee(c), Repo Malepe, Abbubaker Mobara, Lebo Phiri, Deolin Mekoa, Aubrey Modiba; Thabiso Kutumela, Judas Moseamedi.
Swaziland: Mabila, Mdluli, Gamedze, Ndzinsa, Lukhele, Badenhorst, Dlamini, Ndlovu, Ginindza ,Tsabedze, Nhleko.
Nusu fainali ya pili inachezwa leo Alhamisi kati ya Botswana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Leopard ilifuzu katika hatua hiyo kwa ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Msumbiji katika hatua ya robo fainali huku Bostwana ikifuzu kwa kuwaangusha wenyeji Namibia kwa mabao 5 kwa 4 kupitia mikwaju ya penalti.
Fainali itachezwa siku ya Jumamosi.
Zambia na Namibia nazo zitachuana katika fainali ya kuwania taji la Plate, kwa timu ambazo hazikufuzu katika hatua ya nusu fainali.
Licha ya kuondolewa katika hatua ya nusu fainali, Felix Badenhorst anaongoza katika safu ya ufungaji mabao 5.