Wiki hii Shirikisho la soka nchini Misri, lilimteua Javier Aguirre kuwa kocha mpya wa timu ya taufa ya soka.
Raia huyo wa Misri, anachukua nafasi ya Hector Cuper raia wa Argentina, aliyeondoka baada ya Misri kuondolewa mapema katika michuano ya kombe la dunia mwezi uliopita kule Urusi.
Kocha huyu mpya ametia saini mkataba wa miaka miaka, ana kibarua cha kuisaidia Misri kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao nchini Cameroon.
Misri imepangwa katika kundi moja na Tunisia, Niger na Swaziland. Mechi yake ya kwanza, ilifungwa na Tunisia bao 1-0 na mechi ujao ni tarehe saba kati yake na Niger.
Mchezaji wa zamani wa Arsenal Mfaransa Thierry Hery alikuwa anapewa nafasi ya kuwa kocha wa timu hii.