Klabu ya soka ya Al Ahly nchini Misri ina nafasi ya kufuzu katika hatua ya mwondoano kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika ikiwa itaishinda Wydad Casablanca nchini Morocco siku ya Jumatano.
Itakuwa mara ya kwanza kufika katika hatua hiyo baada ya kufanya hivyo mwaka 2013 na kunyakua taji hilo.
Kocha wa Alhly Hossam El Badry ambaye pia ni mchezaji wa zamani amesema mashabiki wa klabu hiyo wanataka ushindi kwa sababu wanaona wamelikosa taji hilo kwa muda mrefu.
Ahly na Zanaco kutoka Zambia zinaongoza kundi la D kwa alama saba baada ya mechi tatu.
Wydad Casablanca ni wa tatu kwa alama tatu huku Coton Sport ya Cameroon ikiwa haina alama katika kundi hilo.
Ratiba kamili:-
Taji la Shirikisho:
-
Klabu bingwa
Kundi A:
Kundi B:
Jumanne: Al Merrikh v Ferroviario Beira
Jumatano : Al Ahly Tripoli v CAPS Utd
Jumatano: Al Hilal v Etoile du Sahel
Jumatano: USM Alger v Zamalek
Kundi C:
Kundi D:
Jumanne: AS Vita Club v Saint George
Jumatano : Coton Sport v Zanaco
Jumatano: Esperance v Mamelodi Sundowns
Jumatano: Wydad Casablanca v Al Ahly