Al Ahly ya Misri, itacheza na Esperance de Tunis, ya Tunisia, katika fainali ya kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika, itakayofanyika mwezi Novemba.
Licha ya kufungwa mabao 2-1 na Entente Setif ya Algeria siku ya Jumanne usiku, ilifuzu kwa jumla ya mabao 3-2 kwa sababu ya ushindi wa nyumbani wa mabao 2-0 zaidi ya wiki tatu zilizopita.
Hii ilikuwa ni mechi ya kwanza kati ya nane zilizopita kwa ya Al Ahly inayofunzwa na kocha Mfaransa Patrice Carteron kupoteza.
Mabingwa hao mara nane wa taji hili, wataanza kuwa wenyeji wa mchuano wa fainali tarehe mbili mwezi Novemba jijini Cairo, kabla ya mechi ya mwisho kuchezwa mjini Rades, tarehe 9.
Esperance de Tunis, nayo ilifuzu baada ya kupata ushindi wa mbao 3-4. Licha ya kufungwa ngenini na Primero de Agosto bao 1-0, ikicheza nyumbani ilifanikiwa kupata ushindi wa manao 4-2.
Mshindi baada ya mechi hizo mbili, atajinyakulia Dola za Marekani Milioni 2.5 na kufuzu kucheza kombe la dunia, baina ya vlabu katika nchi ya Falme za Kiarabu mwezi Desemba.