Shirikisho la soka nchini Algeria limemteua mchezaji wa zamani Djamel Belmadi kuwa kocha wa timu ya taifa.
Amesaini mkataba wa miaka minne.
Belmadi mwenye umri wa miaka 42, anakuwa kocha wa sita wa Algeria ndani ya miaka mwiili na anachukua nafasi ya Rabah Madjer aliyefutwa kazi mwezi Juni.
Aliwahi kuichezea Algeria kati ya mwaka 2000 na 2004 na kuifungia mabao matano katika mara 20 alizocheza.
Mwaka 2004, alikuwa nahodha wa timu ya taufawkaati nchi yake ilipokuwa mwenyeji wa mataifa bingwa barani Afrika.
Kazi kubwa itakuwa ni kuisaidia nchi yake kufzu katika fainali ya Afrika mwakani nchini Cameroon na Algeria ipo katika kundi moja na Benin, Gambia na Togo.