Na Victor Abuso,
Klabu ya AS Vita Club nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndio mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini humo msimu huu.
Ligi kuu ya soka nchini humo ilisitishwa kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili na hivyo kuwapa ushindi vijana wa kocha Florent Ibenge.
Mabingwa wa zamani TP Mazembe ni wa pili huku CS Don Bosco ikiwa katika nafasi ya tatu.
Vlabu hivyo vitatu vimefuzu katika michuano ya klabu bingwa na Shirikisho barani Afrika msimu ujao.
AS Vita Club yenye makao yake jijini Kinshasa, na TP Mazembe yenye makao yake mjini Lubumbashi zitacheza katika michuano ya klabu bingwa huku, Don Bosco ikicheza katika michuano ya Shirikisho.
Kinachosalia msimu huu ni kuwania taji la taifa “Congo Cup” .
Shirikisho la soka Fecofa limetangaza kuwa michuano ya kuwania hilo itaanza tarehe 10 hadi tarehe 23 mwezi Juni mjini Lubumbashi, jijini Kinshasa na mjini Bukavu.
Vlabu vinavyotaka kushiriki katika michuano hii vitahitajika kulipa Dola za Marekani 500 na vile vinavyotaka kushiriki vimepewa saa 72 kuwasilisha maombi yao kwa chama cha soka Fecofa.
Bingwa ni FC MK Etancheite.