Klabu ya AS Vita Club itakuwa na kibarua kigumu siku ya Jumapili jijini Kinshasa, katika fainali ya pili ya kuwania taji la Shirikisho barani Afrika.
Hii ni kutokana na matokeo mabaya ya kufungwa mabao 3-0 na klabu ya Raja Casablanca ya Morocco katika fainali ya kwanza iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Casablanca katika uwanja wa Mohammed wa tano.
Raja Casablanca ilianza vema katika dakika ya 47, baada ya Soufiane Rahimi kupachika bao na kufunga la pili katika dakika 61.
Mambo yalikuwa mabaya zaidi kwa AS Vita Club, baada ya Mahmoud Benhalib kuifungia klabu yake bao la tatu kupitia mkwaju wa penalti.
Raja Casablanca ilishinda taji hili mara moja, mwaka 2003.