Fredrick Nwaka,
Dar es Salaam. Mchezo wa Ligi Kuu baina ya Singida United na Azam umekuwa gumzo huko kila timu ikisema itaibuka mshindi.
Timu hizo zitapambana jumamosi katika Uwanja wa Jamhuri uliopo Mjini Dodoma, Katikati ya Tanzania.
“Ni mechi ngumu lakinj tuko tayari kupambana, kikosi changu kina ari kubw kwa ajili ya mchezo huo,”alisema Idd Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam.
Azam inaongoza ligi kwa kuwa na alama 10.
Naye Kocha mkuu wa Singida United, Hans Pluijm amesema hiyo ni mechi ngumu na dakika 90 zitaamua matokeo ya mchezo.
“Ni mechi ngumu kwa kila timu, tinasubiri dakika tisini,”amesema, raia huyo wa Uholanzi.