Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Timu ya Azam inayofunzwa na Kocha raia wa Romania Aristico Cioaba imeondoka Dar es Salaam kuelekea Mtwara, kusini mwa Tanzania kucheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu.

Ligi ya Tanzania Bara itaanza Jumamosi ambapo Azam itacheza na Ndanda katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Timu hiyo imeondoka na wachezaji wote isipokuwa Shaban Idd anayesumbuliwa na jeraha la mguu.

Kocha Cioaba alisema ana matumaini makubwa ya kushinda mechi hiyo ya kwanza.

“Ni mechi ngumu kwa kuwa msimu uliopita walitufunga kwenye uwanja wao. Timu yangu ina ari kubwa,”alisema Kocha huyo wa zamani wa Raja Casablanca ya Morocco.

Msimu uliopita Azam ilishika nafasi ya nne.

More in