Timu ya Azam inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara imeendelea kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya mashindano mbalimbali msimu ujao.
Klabu hiyo yenye maskani yake Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam imemrejesha kundi kiungo wake wa zamani Mudathiri Yahya ambaye msimu uliopita aliitumikia Singida United.Amesaini mkataba wa miaka miwili.
Kiungo huyo awali alikuwa Azam kabla ya kwenda Singida ambako alicheza kwa mafanikio na kuiwezesha klabu hiyo kufika hatua ya fainali ya michuano ya taji la shirikisho Tanzania na vilevile kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Sports Pesa iliyofanyika nchioni Kenya.
Aidha Azam, imemsajili kiungo Ditram Nchimbi ambaye msimu uliopita aliitumikia Njombe Mji iliyoteremka daraja. Kiungo huyo aliwahi kuitumikia Mbeya City ya Mbeya. Awali ilimsmajili kwa mkataba wa mwaka mmoja mshambuliajin wa zamani wa Yanga, Donald Ngoma.
Azam pia imemnasa kocha msaidizi wa z amani wa yanga, Juma Mwambusi ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, atasaidiana na Hans Pluijm. Makocha hawa waliwahi kufanya kazi pamoja wakiwa Yanga na kuiwezesha klabu hiyo kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu.
Azam imepania kuimarisha kikosi chake baada ya kutofanya vizuri msimu uliopita na kupitia msemaji wake imesema inalenga kuimarisha kikosi chake ili kutwaa mataji msimu unaokuja.