Klabu ya Azam FC imejichimbia Uganda kwa wiki moja sasa ikijiandaa na mashindano ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, msimu ujao.
Kocha wa Azam, Mholanzi Hans Van Pluijm ameiambia RFI Kiswahili kwamba kambi ya timu yake ni nzuri na anaaamini kikosi chake kitawania taji msimu ujao.
“Maandalizi yanakwenda vizuri na wachezaji wote wako sawa, Ngoma pia ameanza mazoezi mepesi na kuna matumaini ya kujumuika naye siku chache zijazo,”
Donald Ngoma aliumia wakati akiitumikia Yanga msimu uliopita na hakuwemo kwenye kikosi cha Azama ambacho kilishinda taji la Kagame wezi uliopita kwa kuifunga Simba mabao 2-1.
Azam kama ilivyo kwa Simba zinatajwa kama klabu zilizofanya usajili mzito kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu na kichuano mingine ya kimataifa.
Baadhi ya nyota hao ni Nicholaus Wadada, Tafadzwa Kutinyu na Mudathir Yahya