Na Mwandishi wetu akiwa Dar Es Salaam,
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania bara kupitia afisa mtendaji mkuu wake Boniface Wambura imetangaza kukubali ombi la Yanga SC la kusogeza mbele kwa siku moja mchezo wao dhidi ya Polisi Tanzania uliokuwa umepangwa kuchezwa Oktoba 2 uwanja wa Uhuru na sasa utachezwa Oktoba 3 2019.
Maamuzi hayo wameyakubali baada ya kujiridhisha kuwa Yanga SC wamerejea nchini kwa makundi wakitokea Zambia walipokuwa wanacheza mchezo wa klabu Bingwa Afrika dhidi ya Zesco na kupoteza mchezo huo kwa mabao 2-1.
“Tunewakubalia ombi lao ni kweli tumefuatilia timu itarudi kwa makundi na itarudi kuanzia leo na wengine kesho kwa hiyo tumeamua kusogeza mbele kwa siku moja, mechi yao badala ya tarehe 2 itachezwa alhamisi ya Oktoba 3 2019” alisema Boniface Wambura
Kundi la kwanza la Yanga SC lilirejea Tanzania likitokea Ndola Zambia alfajiri ya Jumatatu ya Septemba 30 na wengine wameingia Jumanne ya Oktoba 1, kutokana na kukosa muda wa kujiandaa na kupumzika bodi ya Ligi imekubali kusogeza mbele kwa siku moja mchezo wao.