Na Victor Abuso,
Klabu ya ES Setif ya Algeria siku ya Ijumaa itakuwa na mchuano muhimu dhidi ya ndugu zao USM Alger katika mechi muhimu ya hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika.
Mabingwa hao watetezi wa taji hili wapo katika kundi moja na Al-Merrikh ya Sudan na MC El Eulma pia ya Algeria.
Utakuwa ni mchuano wa mwisho wa kundi hili na klabu hii ina alama 4 baada ya michuano minne.
Mshambuliaji wa Setif Mohamed Benyettou ameliambia gazeti la competition.dz kuwa wenzake wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri na kufuzu katika hatua ya mwondoano ya michuano hiyo.
Naye kocha wa USM Miloud Hamadi amesema kuwa licha ya mchezaji wake wa kutegemewa Farouk Chafaï kujeruhiwa na Rabie Meftah, ambaye alipewa adhabu ya kutocheza katka mchuao huo.
Setif nayo, ina wasiwasi wa beki wao Mohamed Bouchar pamoja na viungo wao wa kati Ibrahim Amada na Sid Ali Lamri.
Nayo klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo ipo katika kundi A pamoja na Moghreb Tetouan ya Morocco, Al Hilal ya Sudan na Smouha ya Misri, itakuwa jijini Khartoum mwishoni mwa juma hili kumenyana na Al Hilal.
Mabingwa hao wa zamani wanaongoza kundi hilo kwa alama 8.
Vlabu viwili katika kila kundi yatafuzu katika hatua ya nusu fainali ya michuano hii.
Al Hilal ya Sudan, Smouha ya Misri, Es Setif na MC El Eulma zipo hatarini kutofuzu katika michuano hiyo.