Fainali ya kwanza kuwania taji la Shirikisho barani Afrika itachezwa Jumamosi kati ya klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini na Etoile du Sahel ya Tunisia.
Fainali hiyo ya kwanza itachezwa katika uwanja wa Orlando, huku fainali ya pili ikiratibiwa kuchezwa tarehe 29 ugenini jijini Tunis nchini Tunisia.
Mabingwa watetezi Al Ahly kutoka Misri, walibanduliwa nje katika michuano hii ambayo vlabu kutoka Tunisia imekuwa ikitamba kwa muda mrefu katika mashindano haya barani Afrika.
CS Sfaxien ndio klabu iliyofanikiwa sana katika mashindano haya ya Shirikisho kwa kushinda mataji matatu mwaka 2007, 2008, 2013 na mwaka 2010 waliibuka katika nafasi ya pili.
Klabu ya Etoile du Sahel ilishinda taji hili mwaka 2006 na kumaliza wa pili mwaka wa 2008.
Hakuna klabu ya Afrika Kusini ambayo imewahi kushinda taji hili. Vlabu vingine vilivyowahi kushinda taji hili ni pamoja na FAR Rabat, Hearts of Oak ya Ghana, Stade Malien ya Mali, Mas Fez ya Morroco na AC Leopards ya Congo Brazaville.
Mshindi wa taji hili mbali na kupata kombe, atakabidhiwa pia Dola za Marekani Laki 625