Mechi za nusu fainali kuwania taji la Shirikisho barani Afrika zinachezwa siku ya Jumatano.
Enyimba ya Nigeria itafungua mchuano wa mapema, kati ya Raja Casablanca ya Morocco.
Al Masry ya Misri itakuwa nyumbani kumenyana na AS Vita Club ya DRC.
Enyimba ambayo mara ya mwisho kushiriki katika mashindano haya ilikuwa mwaka 2010 na kuondolewa katika hatua ya 16 bora.
Mwaka huu, ilifuzu katika hatua hii baada ya kuishinda Rayon Sport ya Rwanda katika hatua ya robo fainali.
Raja Casablanca nayo ilifuzu baada ya kuishinda CARA Brazaville katika mchuano wa robo fainali.
AS Vita Club inakwenda katika mechi hii ikiwa na historia ya kushiriki katika mashindano haya mara tatu, mwisho ikiwa ni mwaka 2010.
Mbali na michuano hii, siku ya Jumanne kulikuwa na mechi mbili za mzunguko wa kwanza kuwania taji la klabu bingwa.
Mabingwa mara nane wa taji hili, Al-Ahly ilianza vema nyumbani baada ya kuishinda ES Setif ya Algeria mabao 2-0.
Primero de Agosto ya Angola, nayo ilianza vema baada ya kuifunga Esperance de Tunis, ya Tunisia bao 1-0.
Mechi ya marudiano itachezwa tarehe 23 mwezi huu.