Klabu ya soka ya Yanga FC ya Tanzania ilianza vibaya michuano ya hatua ya makundi kuwania taji la Shirikisho barani Afrika.
Wakicheza ugenini katika mechi ya kundi D, Yanga walifungwa mabao 4-0 na USM Alger katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Juillet 5 jijini Algiers.
Mabao ya USM Alger, yalifungwa na Oussama Darfalou katika dakika ya nne ya mchuano huo.Wengine waliofunga mabao ni pamoja na Farouk Chafai, Abderrahmane Meziane na Mohamed Lamine Zemmamouche.
Rayon Sport ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya nao, walianza kwa sare katika mchuano wake wa kwanza katika uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali.
Gor Mahia ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia mshambuliaji Meddie Kagere katika dakika 11 ya mchuano huo huku Eric Rutanga, akisawazisha katika dakika ya 24 ya mchuano huo.
Kundi hili linaongozwa na USM Alger kwa alama tatu, huku Gor Mahia na Rayon Sport wakiwa na alama 1.
Young Africans au Yanga hawana alama.
Ratiba ya mechi zajizo:-
Tarehe 16 mwezi Mei mwaka 2018
Young Africans vs Rayon Sport
Gor Mahia vs USM Alger.
Matokeo mengine:
Kundi C:-
Enyimba (Nigeria) 2-0 Djoliba (Mali)
Williamsville AC (Ivory Coast 1-0 CARA Brazaville (Congo)
Kundi B:-
RS Berkane (Morocco) 1-0 Al-Hilal (Sudan)
Al-Masry (Misri) 2-0 UD Songo (Msumbiji)
Kundi A:-
ASEC Mimosas (Cote Dvoire) 1-0 Aduana Stars (Ghana)
Raja Casablanca (Morocco) 0-0 AS Vita Club (DRC)
Michuano ya klabu bingwa barani Afrika, nayo ilichezwa mwishoni mwa wiki iliyopita:-
Kundi A:-
Township Rollers ya Bostwana ilianza vema baada ya kuifunga KCCA ya Uganda bao 1-0 nyumbani na sasa inaongoza kundi hili kwa alama tatu.
Al-Ahly ambao haikufungana na Esperance de Tunis ya Tunisia, ina alama moja.
Kundi B:-
Mabingwa wa mwaka 2015 TP Mazembe, ilianza vema baada ya kusihinda ES Setif ya Algeria mabao 4-1, huku MC Alger ikitoka sare ya bao 1-1 na Difaa El Jadidi ya Morocco.
Kundi C:-
Horoyo ya Guinea nayo ilianza vema baada ya kuifunga AS Togo Port mabao 2-1.
Mabingwa wa mwaka 2016, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, walitoka sare ya bao 1-1 na Wydad Casablanca ya Morocco.
Kundi D:-
Hakuna timu iliyopata ushindi katika kundi hili. ZESCO United wakicheza nyumbani, walipata sare ya bao 1-1 na Mbabane Swallows ya Swaziland.
Mambo yalikuwa vivyo hivyo kati ya Desportivo de Agosto ya Angola dhidi ya Etoille du Sahel ya Tunisia.