Na Victor Abuso,
Shirikisho la soka barani Africa CAF, linasema Joseph Sepp Blatter atakumbukwa sana kwa kulisaidia bara la Afrika kuinua kiwango chake cha mchezo wa miguu.
Rais wa CAF ambaye pia ni Naibu rais wa FIFA Issa Hayatou amesema kuwa CAF inaheshimu uamuzi wa Blatter kujiuzulu na inaunga mkono mabadiliko katika Shirikisho hilo.
“Shirikisho la soka barani Afrika linaheshimu na kutambua kujiuzulu kwa Joseph Sepp Blatter,” Hayatou alisema kupitia taarifa uliochapishwa katika mtandao wa CAF.
Tangu kutangaza kujiuzulu, viongozi wa vyama mbalimbali barani Afrika wamekuwa wakionesha masikitiko makubwa kwa hatua hiyo kwa kile wanachokisema kuwa Blatter ndiye aliyekuwa tegemeo lao.
Rais wa Shirikisho la soka nchini Kenya Sam Nyamweya amedokeza kuwa anaamini kuwa bara la Afrika litampigia kura mtu atakayependekezwa na Blatter.
“Nimeshangazwa na hatua ya Blatter lakini tutaendelea kumuunga mkono na kumpigia kura yule atakayemchagua yeye,” alisema
Nyamweya ameongezea kuwa, “ Tunaamini kuwa kura tulizompa Blatter, tutampa mgombea mwingine,”.
Kiongozi huyo wa soka nchini Kenya amemsifu Blatter kwa kuisaidia Kenya kuanzia miradi ya kuinua soka hasa kwa vijana kwa kuhakikisha kuwa fedha zinapatikana.
Said El Mamry rais wa zamani wa Shirikisho la soka nchini Tanzania na mjumbe wa zamani wa FIFA na CAF amesema binafsi kama mtu aliyefanya kazi na Blatter kwa muda mrefu, hatua hiyo ni pigo kwa bara la Afrika.
“Siku hizi ukitembea katika mataifa mbalimbali barani Afrika utaona Ofisi nzuri nzuri za mashirikisho ya soka, viwanja vya nyasi ya bandia na mambo mengine mazuri, hiyo ni kazi ya Blatter,” alisema El Mamry.
Blatter alitangaza kujiuzulu siku ya Jumatatu kwa kile alichokisema kuwa hawezi kuendelea kuongoza kutokana na kundi la watu wanaompinga.
Uchaguzi mpya unatarajiwa kufanyika mwezi kati ya mwezi Desemba mwaka huu na mwezi Machi mwakani.
Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com
CAF Confederation Cup
Simba snatch late winner against CS Sfaxien as Enyimba beaten
CAF Champions League
Sundown CL campaign has a pulse after beating Raja
CAF Champions League
Sundown CL campaign has a pulse after beating Raja
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...