Kenya, imefuzu katika fainali ya bara Afrika katika mchezo wa soka mwaka 2019.
Hili limetangazwa rasmi na Shirikisho la soka barani Afrika CAF, baada ya kuiondoa Sierra Leone, kwenye michuano ya kufuzu.
Hatua hii imechukuliwa kwa sababu, Sierra Leone imefungiwa na Shirikisho la soka duniani FIFA, baada ya serikali yao kuingilia masuala ya usimamizi wa soka nchini humo, kinyume na kanuni za Shirikisho hilo.
Wakenya wamefurahishwa na tangazo hili la CAF, huku rais Uhuru Kenyatta akisema kuwa, ni hatua nzuri sana kwa mchezo wa soka nchini humo na kuahidi serikali kuisaidia Harambee Stars.
Mara ya mwisho kwa Kenya, kushiriki katika michuano hii ya bara Afrika, ilikuwa ni mwaka 2004 nchini Tunisia.
Kwa mara ya kwanza, mataifa 24 yashiriki katika michuano hiyo.
Kuelekea AFCON 2019, haijafahamika mwenyeji wa michuano hii.
Wiki iliyopita, CAF iliipokonya Cameroon haki za kuwa mwenyeji kwa sababu ya maandalizi mabaya likiwemo suala tata la usalama.