Shirikisho la soka barani Afrika, limethibitisha kuwa timu ya taifa ya Guine Bissau itashiriki katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao nchini Gabon.
Hatua hii imekuja baada ya Zambia kulalamika kuwa, kipa wa Guinea Bissau Papa Massa Mbaye Fall hakustahili kuichezea nchi hiyo, kwa sababu aliwahi kuichezea Senegal katika michuano hii.
Hata hivyo, CAF inasema baada ya uchunguzi wake, imebaini kuwa madai ya Zambia sio kweli na kipa huyo hakuwahi kuichezea wala kusajiliwa na Shrikisho la soka nchini Senegal.
Hii habari mbaya kwa mabingwa wa mwaka 2012 Zambia, ambayo hataifuzu kucheza fainali ya mwakani.
Guinea Bissau ambayo inaongoza kundi la E kwa alama 10, itamenyana na Congo Brazil katika mechi ya mwisho huku Zambia ambayo ni ya pili kwa alama sita ikijiandaa kumenyana na Kenya.