Connect with us

CAF:Mzunguko wa pili wa klabu bingwa na Shirikisho

CAF:Mzunguko wa pili wa klabu bingwa na Shirikisho

 

Mwishoni mwa juma hili,michuano ya awali ya klabu bingwa na Shirikisho, mzunguko wa pili zinachezwa katika viwanja mbalimbali barani Afrika.

Mabingwa mara mbili wa zamani wa taji la klabu bingwa barani Afrika Enyimba FC ya Nigeria itakuwa na kibarua cha kubadilisha matokeo dhidi ya SC Vipers ya Uganda.

Vipers ambayo inashiriki katika mashindano haya kwa mara ya kwanza, wiki mbili zilizopita iliishinda Enyimba bao 1 kwa 0 jijini Kampala na siku ya Jumapili watarudiana na mabingwa hao mara saba wa Nigeria mjini Port Harcourt.

SC Vipers inahitaji sare ili kufuzu katika mzunguko wa kwanza wa mashindano haya lakini Enyimba nayo inahitaji ushindi wa angalau mabao 2 kwa 0 kujikatia tiketi.

Mshindi atamenyana na mshindi kati ya Lilo FC ya Lesotho au Vital’O ya Burundi katika mzunguko wa kwanza mwezi ujao wa Machi.

Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini pia ni klabu nyingine itakayokuwa nyumbani na inahitaji kuutumia uwanja wake ili kupata matokeo mazuri.

Mchuano wa kwanza, klabu ya Chicken Inn kutoka Zimbabwe walipata ushindi wa bao 1 kwa 0 mjini Bulawayo.

Kipa wa Mamelodi Sundowns Denis Onyango kutoka Uganda amesema ana uhakika klabu yake itapata ushindi katika mhcunao huo utakaopigwa Jumamosi usiku jijini Pretoria.

Ratiba nyingine klabu bingwa barani Afrika.

Yanga FC (Tanzania) Vs Cercle de Joachim ( Mauritania)

Mbabane Swallows(Swaziland) vs APR(Rwanda)

CnaPS Sport( Madagascar) vs Gor Mahia ( Kenya)

AS Vita Club (DRC) vs Mafunzo FC ( Zanzibar)

Ratiba ya taji la Shirikisho barani Afrika

Atlabara (Sudan Kusini) vs Police ( Rwanda)

Bandari FC ( Kenya) vs FC Saint Eloi Lupopo (DRC)

Atletico Olympic ( Burundi) vs Fomboni Club ( Comoros)

Sport Club Villa (Uganda) vs Al Khartoum (Sudan)

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in