Connect with us

 

Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini itamenyana na Zamalek ya Misri katika fainali ya msimu huu kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika CAF.

Sundowns ilifuzu baada ya kupata ushindi wa jumla ya mabao 3-2 katika mchuano wa marudiano ya nusu fainali mwishoni mwa wiki iliyopita, baada ya kuifunga ZESCO United ya Zambia.

Zamalek ya Misri nayo ilifuzu kibahati kwa ushindi wa jumla ya mabao 6-5 dhidi Wydad Casablanca ya Morocco baada ya mchuano wa marudiano.

Fainali kati ya vlabu hivi viwili nyumbani na ugenini mwezi Oktoba.

Timu hizi mbili zinakutana tena baada ya kufanya hivyo katika hatua ya makundi mwezi Julai.

Katika mchuano huo wa hatua ya makundi, Zamalek wakiheza nyumbani mjini Cairo, walifungwa na Mamelodi Sundowns mabao 2-1, huku mchuano wa marudiano, Sundowns wakiendeleza ubabe wao kwa kupata ushindi wa bao 1-0 nyumbani.

Zamalek imewahi kushinda taji hili mara 5, mwaka 1984, 1986,1993,1996 na 2002. Mamelodi Sundowns haijawahi kushinda taji hili.

TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo nayo itachuana na MO Bejaia ya Algeria katika fainali ya kuwania taji la Shirikisho barani Afrika.

Mazembe walifika katika hatua hiyo kwa faida ya bao la ugenini walipotoka sare kwa bao 1-1 dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia ambao ndio walikuwa wanashikilia taji hilo.

MO Bejaia nayo pia ilifuzu katika hatua hiyo pia kwa faida ya bao la ugenini baada ya kutoka sare ya kutofungana katika mchuano wa kwanza na kutoka sare ya bao 1-1 mwishoni mwa wiki iliyopita.

Timu hizi pia zinakutana baada ya kufanya hivyo katika hatua ya makundi, na Mazembe kupata sare ya kutofungana katika mchuano mmoja na Mazembe kupata ushindi wa bao 1-0 katika mchuano wa marudiano.

More in