TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumapili hii,inaikaribisha MO Bejaia ya Algeria mjini Lubumbashi, kupambana katika fainali ya pili kutafuta bingwa wa taji la Shirikisho barani Afrika.
Mazembe inakwenda katika fainali hii ikiwa na bao la ugenini baada ya fainali ya kwanza mwishoni mwa wiki iliyopita, timu zote mbili kutoka sare ya bao 1-1.
Shirikisho la soka barani Afrika limewateua Marefarii watatu kutoka Senegal watakaocheza mechi hiyo muhimu.
Marefarii hao pamoja na Malang Diedhiou atakayekuwa mwamuzi wa kati, akisaidiwa na wenzake Djibril Camara na El Hadji Malick Samba.
Mambo muhimu ya kufahamu kuelekea katika mchezo huu:-
-Mazembe imefunga mabao 14 katika mechi 11 ilizocheza katika michuano hii huku Mo Bejaia ikifunga mabao 5.
-Vlabu kutoka Tunisia na Morocco vimekuwa vikishinda mataji ya fainali hii kwa muda wa miaka 12 iliyopita.Timu kutoka Tunisia zimeshinda mara 5, kutoka Morocco mara 3.
–Mshindi wa taji hili atapokea Dola za Marekani 660,000 huku atakayeibuka wa pili akipata Dola za Marekani 462,000.
–Bingwa atacheza fainali ya Super Cup dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini iliyoshinda taji la klabu bingwa barani Afrika msimu huu.
-Mwaka 2006 klabu ya Etoile Sahel kutoka Tunisia ilishinda taji hili kwa kutofungwa mchuano wowote. Ilishinda mechi nane na kutoka sare mara mbili.
Wafungaji bora katika michuano ya mwaka huu
–Mabao 6 – Cabungula (Sagrada Esperanca kutoka Angola ), Rainford Kalaba (TP Mazembe DRC)