Connect with us

 

Nigeria na Cameroon zitachuana katika fainali ya kutafuta bingwa wa bara Afrika katika mchezo wa soka baina ya wanawake.

Super Falcons, ambao ndio mabingwa watetezi, walifuzu katika hatua hiyo baada ya kuishinda Banyana Banyana ya Afrika Kusini bao 1-0 katika mchuano wa nusu fainali Jumanne usiku.

Bao hilo la Nigeria lilitiwa kimyani na Desire Oparanozie licha ya Afrika Kusini kuanza vema kutawala mchuano huo lakini ikashindwa kutumia nafasi yao kufunga mabao.

Wenyeji wa michuano hii nao walijinyakulia ushindi katika mchuano wa kwanza dhidi ya Ghana.

Mchuano huu ulitawaliwa kwa kiasi kikubwa na Ghana lakini bao la Raissa Feudijo katika dakika ya 71, liliwababatiza mabeki wa Ghana.

Hii itakuwa ni fainali ya tatu kati ya Cameroon na Nigeria katika historia ya michuano hii ambayo Nigeria imeshinda mara saba na sasa inatafuta taji lake nane.

Fainali ya kwanza, kati ya mataifa haya miwili ilichezwa mwaka 1991, 2002 na 2004.

Katika fainali hizo zote, Nigeria iliishinda Cameroon. Je mwaka huu mambo yatakuwaje ?

Jibu ni siku ya Jumamosi katika fainali itakayochezwa katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo siku ya Jumamosi jijini Yaounde.

More in AWCON