Cameroon, mabingwa wa mwaka 2003 katika taji la soka barani Afrika kwa vijana wasiozidi miaka 17, wameanza vema mashindano yanayoendelea nchini Tanzania.
Lions Indomptables waliifunga Guinea mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Morocco na Senegal nazo zilitoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya pili ya kundi B.
Cameroon inaongoza kundi la B kwa alama tatu huku Morocco, Senegal na Guinea zikiwa na alama moja.
Michuano hii itarejelewa siku ya Jumatano.
Nigeria inayoongoza kundi la A kwa alama tatu, itamenyana na Uganda baada ya kuwashinda wenyeji Tanzania mabao 5-4.
Tanzania nayo itachuana na Angola, ambayo mechi ya kwanza iliishinda Uganda bao 1-0.