-
-
by
Victor Abuso
Shirikisho la soka nchini Tanzania linasema halitakuwa katika nafasi ya kuandaa wa michuano ya mwaka huu ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati CECAFA.
TFF ilikuwa imeahidi kuchukua nafasi ya Zanzibar iliyopewa jukumu hilo lakini ikajiondoa kwa ukosefu wa fedha.
Rais wa TFF Jamal Malinzi kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema, nchi yake haitaweza kuwa mwenyeji wa michuano hiyo kwa sababu ya msongamano wa mechi za Kimataifa jijini Dar es salaam baada ya Yanga FC kufuzu kucheza hatua ya makundi kuwania taji la Shirikisho.
“Shirikisho la soka nchini Tanzania, halitaandaa michuano ya klabu bingwa ya CECAFA mwaka 2016, kwa sababu ya msongamano wa ratiba ya kimataifa,” alisema Malinzi.
Michuano hii inafadhiliwa na rais wa Rwanda Paul Kagame, amekuwa akifadhili michuano hii tangu mwaka 2002, imepangwa kufanyika kuanzia katikati ya mwezi wa Julai hadi mwanzoni mwa mwezi wa Agosti.
Mwaka 2015 michuano hii inayofahamika kwa jina maarufu la Kagame Cup ilifanyika nchini Tanzania na wenyeji Azam FC wakayakua ubingwa kwa kuwashinda Gor Mahia ya Kenya mabao 2 kwa 0 katika fainali.
Tanzania imeandaa michuano hii mara tatu kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, hii ikitokana na idadi kubwa ya mashabiki wengi kujitokeza uwanjani.
Mara ya mwisho Kenya kuandaa michuano hii ilikuwa ni mwaka 2001, wakati huo vlabu vyote vya Kenya vilifika fainali, Tusker FC na Oserian Fastac na baada ya mikwaju ya penalti, Tusker wakanyakua taji hilo.



CAF Confederation Cup
Simba book final spot in CAF Confederation cup

CAF Confederation Cup
Simba book final spot in CAF Confederation cup
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 5 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...