Connect with us

CHAN 2016: Je, itakuwa ni DRC au Mali Jumapili ?

CHAN 2016: Je, itakuwa ni DRC au Mali Jumapili ?

DRC FANSS

Mali Mali

Timu ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kesho Jumapili itachuana na Mali, katika fainali ya kutafuta bingwa wa Afrika wa mashindano yanayowashirikisha wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN.

Mchuano huu utachezwa kuanzia saa moja na nusu saa za Afrika Mashariki, huko Afrika ya Kati itakuwa ni saa kumi na mbili na nusu, katika uwanja wa Amahoro jijini Kigali nchini Rwanda.

Leopard ya DRC ambao ni mabingwa wa mwaka 2009, ilifuzu katika fainali juma hili baada ya kuifunga Syli National ya Guinea kwa mabao 5 kwa 4 baada ya kupigwa penalti baada ya timu zote mbili kutoka sare ya bao 1 kwa 1 katika muda wa kawada na ule wa ziada.

1453326029DR-Congo-players-celebrate-one-their-goals-against-Ethiopia-in-the-first-match-on-Sunday.-S

Mali nayo ilifuzu baada ya kuifunga Ivory Coast bao 1 kwa 0.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inalenga kuwa timu ya kwanza kushinda taji hili la CHAN kwa mara ya pili tangu kuanza kwake mwaka 2009 nchini Ivory Coast.

Maelfu ya mashabiki wa Leopard wamekuwa wakiwasili jijini Kigali kushuhudia fainali hiyo , na kocha Florent Ibenge atakuwa anawategemea wachezaji kama kipa Ley Matampi, Padou Boumpunda bila kumsahau nahodha Joel Kimwaki.

Eagles ya Mali nayo inacheza fainali ya kwanza ya CHAN, ikiwa haijafungwa mchuano hata mmoja katika mashindano haya, na ilifanikiwa kuishinda, Ivory Coast na Tunisia.

Mali itakabiliana na DRC bila ya mchezaji wake wa kutegemewa, kiungo wa kati Sekou Diarra, ambaye alipewa kadi nyekundu lakini kijana chipukizi Abdoul Dante mwenye umri wa miaka 17 atakuwa anategemwa sana katika safu ya Mali.

Mali fans

Kabla ya mchuano huo wa fainali, Tembo wa Ivory Coast watamenyana na Syli National wa Guinea kutafuta nafasi ya tatu katika mashindano haya.

Hadi sasa mechi, 30 zimechezwa katika michuano hii ya CHAN na mabao 74 kufungwa.

Wachezaji wanaoongoza katika ufungaji wa mabao ni pamoja na Chisom Chikatara kutoka Nigeria, Ernest Sugira kutoka Rwanda, Ahmed Akaichi na Saada Bgur wote kutoka Tunisia wote ambao wamefunga mabao manne.

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in