CS Constantine ya Algeria ndio klabu pekee ambayo imepata ushindi katika mechi mbili ambazo imecheza hadi sasa, katika harakati za kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, CS Constantine iliishinda TP Mazembe ya DRC mabao 3-0 katika mechi yake ya pili iliyocheza nyumbani katika uwanja wa Mohamed Hamlaoui.
Mechi ya kwanza, iliishinda Club Africain ya Algeria bao 1-0 mjini Sousse wiki mbili zilizopita.
Klabu hii inaongoza kundi la C kwa alama sita, ikifuatwa na Club Africain na TP Mazembe ambazo zina alama moja, huku Ismaily ya Misri ikiwa ya mwisho bila alama.
Matokeo mengine, Kundi A:-
ASEC Mimosas (Ivory Coast) 1-0 Lobi Stars (Nigeria)
Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) 2-1 Wydad Casablanca (Morocco)
Kundi B:-
Esperiance de Tunis (Tunisia) 2-0 FC Platinum (Zimbabwe)
Orlando Pirates (Afrika Kusini) 3-0 Horoya (Guinea)
Kundi D:-
JS Saoura (Algeria) 1-1 Al-Ahly (Misri)
AS Vita Club (DRC) 5-0 Simba (Tanzania)