Rais wa Shirikisho la Soka nchini Afrika Kusini SAFA, Dr. Danny Jordan ametetea tena kiti chake baada ya kuchaguliwa bila kupingwa kuongoza shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 66 alipata kura za ndio 234 kati ya wajumbe 246 walioshiriki katika uchaguzi huo.
Jordan anakabiliwa na tuhuma za unyanyasi wa kingono anazodaiwa kuzitekeleza miaka 25 iliyopita dhidi ya mwimbaji na mbunge wa zamani Jennifer Ferguson lakini wajumbe wa mkutano wa uchaguzi wamemchagua tena kuongoza shirikisho hilo.
Uchaguzi huo umefanyika licha ya mahaka kujaribu kuusimamisha na Jordan amesema uchaguzi huo ulifuata taratibu zote za kisheria.
Jordan alikuwemo kwenye kamati ya maandalizi iliyofanikisha Afrika Kusini kuandaa fainaliza Kombe la dunia mwaka 2010 na pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la Soka Barani Afrika CAF.