Connect with us

 

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limetangaza droo ya hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa na Shirikisho mwaka huu.

Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini ambao ni mabingwa watetezi wa michuano ya klabu bingwa, wamepangwa katika kundi la C pamoja na Esperance de Tunis ya Tunisia, AS Vita Club ya DRC na Saint George ya Ethiopia.

Zanaco FC kutoka Zambia, wamepangwa pamoja na mabingwa wa zamani Al-Ahly ya Misri, Wydad Casablanca ya Morccco na Coton Sport ya Cameroon.

Kundi B, linawakutanisha Zamalek ya Misri, USM Alger ya Algeria, Al-Ahli Tripoli ya Libya na CAPS United ya Zimbabwe.

Mabingwa wa mwaka 2007 Étoile Sportive du Sahel ya Tunisia, imepangwa katika kundi la A na Al-Hilal ya Sudan pamoja na ndugu zao Al-Merrikh na Ferroviario Beira ya Msumbiji.

Mechi za hatua ya makundi zitachezwa nyumbani na ugenini kati ya mwezi Mei na Julai mwaka huu na mshindi wa kwanza na wa pili, watafuzu katika hatua ya robo fainali.

Michuano ya hatua ya makundi kutafuta taji la Shirikisho pia itaanza mwezi Mei.

Hatua ya makundi:-

Kundi A: FUS Rabat ( Morocco), Club Africain (Tunisia), Rivers United (Nigeria), KCCA (Uganda).

Kundi B: CS Sfaxien (Tunisia), Platinum Stars(Afrika Kusini), MC Alger (Algeria), Mbabane Swallows (Swaziland).

Kundi C: Zesco United (Zambia), Recreativo do Libolo (Angola), Al Hilal Al-Ubayyid (Sudan), Smouha ( Misri).

Kundi D: TP Mazembe (DRC), SuperSport United( Afrika Kusini), Horoya (Guinea), CF Mounana (Gabon).

More in