Droo ya hatua ya makundi ya kutafuta ubingwa taji la klabu bingwa barani Afrika katika mchezo wa soka itatangazwa tarehe 24 mwezi Mei.
Vlabu nane ambavyo vimefuzu katika hatua hii tayari vimefahamika na vitawekwa katika hatua ya makundi mawili, kila kundi na timu nne.
Kanuni za Shirikisho la soka barani Afrika CAF, zinaweka wazi kuwa mechi hizo zitachezwa nyumbani na ugenini na mshindi atafuzu katika hatua ya nusu fainali.
Vlabu vilivyofuzu ni pamoja na:-
- ES Setif ya Algeria
- AS Vita Club ya DRC
- Al-Ahly ya Misri
- Zamalek ya Misri
- ASEC Mimosas ya Cote Dvoire
- Wydad Casablanca ya Morocco
- Enyimba ya Nigeria
- ZESCO United ya Zambia
Mabingwa watetezi wa taji hili msimu uliopita TP Mazembe waliondolewa baada ya kufungwa ugenini mabao 2 kwa 0 na sare ya bao 1 kwa 1 mjini Lubumbashi siku ya Jumatano.
Nayo droo ya hatua ya mwondoano kuwania taji la Shirikisho itafanyika tarehe 21 mwezi Aprili.
Vlabu vilivyofuzu katika michuano hii ya Shirikisho vitakutana na vile vilivyoondolewa katika hatua ya taji la klabu bingwa barani Afrika.
|
Kutoka taji la klabu bingwa |