Droo ya mashindano ya Afrika baina ya wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN yatakayofanyika mwaka 2016 nchini Rwanda imetolewa.
Mataifa kumi na sita yatashiriki katika michuano hiyo na yamepangwa katika makundi manne.
Wenyeji Rwanda wamewekwa katika kundi A na Gabon, Morocco na Ivory Coast na kundi hili litacheza katika uwanja wa Amahoro jijini Kigali.
Mabingwa wa mwaka 2009, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wako katika kundi B na Angola iliyofika fainali mwaka 2011 Angola, Camerooon na Ethiopia na watapiga kambi katika uwanja wa Butare.
Kundi la C lina mabingwa wa mwaka 2011 Tunisia, Nigeria, Niger na Guinea ambao wanacheza kwa mara ya kwanza michuano yao itachezwa katika uwanja wa Nyamirambo.
Uwanja wa Gisenyi utakuwa na kundi D ambao ni pamoja na Zimbabwe, Mali, Uganda na Zambia.
Michuano hii itaanza tarehe 16 mwezi Januari na kumalizika tarehe 7 mwezi Februari.