Mlinda mlango wa kimataifa wa Misri, Essam El Hadary ametangaza kustaafu soka la kimataifa, miezi miwili baada ya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mchezaji mwenye umri miubwa kuwahi kucheza fainali za Kombe la dunia.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 45 anastaafu kucheza soka la kimataifa akiwa ameitumikia Timu ya Taifa ya misri, michezo 159 na kushinda mataji manne ya mataifa ya Afrika na pia akiwa ameifungia nchi yake bao moja.
Aidha meweka rekodi ya kuwa mchezaji mkongwe kuokoa penati katika fainali za kombe la dunia, alicheza mkwaju wa penati katika mchezo wa mwisho wa kundi A baina ya Misri na Saudi Arabia.