Kipa wa timu ya taifa ya soka ya Misri, Essam El-Hadary ameweka historia kwa kuwa mchezaji wa kwanza kushiriki katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika akiwa na umri mkubwa wa miaka 44.
El-Hadary aliweka rekodi hiyo baada ya kuingia uwanjani wakati wa mchuano dhidi ya Mali siku ya Jumanne usiku uliomalizika sare ya bao 0-0.
Mkongwe huyo aliingia uwanjani baada ya kipa wa kwanza wa Ahmed El-Shenawy kupata jeraha na kulazimika kuingia uwanjani.
Wapenzi wa soka wamempongeza sana El-Hadary kwa hatua hii, pongezi ambazo pia amezipata kutoka kwa Shirikisho la soka duniani FIFA.
Hii imekuwa mechi yake ya 148 kuichezea timu ya taifa tangu mwaka 1996.
El-Hadary alishinda taji hili la Afrika mara ya nne mwaka 1998, 2006, 2008 na 2010.