Connect with us

 

Klabu ya St George inamenyana na mtani wake wa jadi Ethiopia Coffee katika mchuano muhimu wa ligi kuu ya soka nchini Ethiopia.

Mchuano huu unapigwa katika uwanja wa Yidenkachew Tessema jijini Addis Ababa.

Mechi kati ya vlabu hivi viwili pinzani nchini humo, imepewa jina maarufu la Sheger derby na kuwa miongoni mwa mechi kubwa barani Afrika.

Kuelekea katika mchuano huu mkubwa, St George wanaongoza msimamo wa ligi kuu kwa alama 42 baada ya kucheza 21 huku Ethipia Coffee ikiwa ya nne kwa alama 35 baada ya mechi 22.

Kati ya mechi zote ilizocheza, St.George imeshinda mechi 12 huku Ethiopia Coffee ikishinda mechi 9 msimu huu.

Mechi ya mzunguko wa kwanza hata hivyo, Ethiopian Coffee ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya St.George.

Saint George Sports Club, ambayo pia inafahamika kama Kedus Giorgis ilianzishwa mwaka 1935.

Imeshinda ligi kuu ya soka nchini humo mara 28, huku mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 2016. Hata hivyo, tangu mwaka 2014, imeshinda mfululizo.

Ethiopia Coffee FC nayo ilianzishwa mwaka 1976 na imeshinda ligi mara mbili mwaka 1997 na 2011.

Historia inaonesha kuwa licha ta kuwa timu pinzani kwa St.George, imekuwa ikabiliwa na changamoto za kifedha na kushindwa kuwasajili wachezaji imara na hata kutoka nje ya nchi.

Ligi kuu ya soka nchini Ethiopia ina vlabu 16.

More in East Africa