Connect with us

 

Timu za taifa za mchezo wa soka za Uganda, Guinea Bissau na Zimbabwe zimeweka historia ya aina yake kufuzu katika fainali ya michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon baada ya kumalizika kwa michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Uganda imefuzu baada ya kucheza katika fainali hii kwa mara ya kwanza na mara ya mwisho mwaka 1978 nchini Ghana, na wakati huo walifungwa na wenyeji mabao 2-0 katika mchuano wa fainali jijini Accra.

Kurejea katika michuano hii mikubwa barani Afrika baada ya kuifunga Comoros bao 1-0 na kufuzu ni hatua kubwa sana ambayo imeleta hisia kubwa nchini humo pamoja na ukanda wa Afrika Mashariki.

Guinea Bissau nayo imeweka historia kwa sababu kwa mara ya kwanza imefuzu kucheza katika michuano hii baada ya kumaliza katika nafasi ya kwanza katika kundi lake kwa alama 10 mbele ya Congo, Zambia mabingwa wa mwaka 2012 na Kenya.

The Warriors ya Zimbabwe nayo inarejea katika soka la bara Afrika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2006.

Zimbabwe ambayo sasa imefuzu mara tatu katika historia ya mashindano haya mwaka 2004 na 2006 na kufika katika hatua ya makundi.

Ilifanikiwa baada ya kumaliza nafasi ya kwanza katika kundi L mbele ya Swaziland, Guinea na Malawi.

Mabingwa mara saba wa taji hili, taji ambalo halijafikiwa na yeyote, Misri, nayo imerejea baada ya mara ya mwisho kushiriki mwaka 2010.

Pharaos kama wanavyojuliana, wanashiriki mara 23 sasa mbele ya Ivory ambayo pia imefuzu na itakuwa inashiriki kwa mara ya 22.

Mataifa mengine yaliyofuzu ni pamoja na wwnyeji Gabon, Morocco, Algeria, Cameroon, Senegal,Ghana, Mali, Burkina Faso, Tunisia, DR Congo na Togo.

DR Congo sasa imefuzu mara 18 na ilinyakua taji hili mwaka 1968 na 1974.

Droo ya michuano hii hatua ya makundi itafanyika tarehe 19 mwezi Oktoba jijini Libreville nchini Gabon.

More in