Shirikisho la soka nchini Rwanda FERWAFA linamtafuta kocha mpya wa timu ya taifa Amavubi Stars.
Gazeti la Times Sports nchini humo limeripoti kuwa, rais wa Ferwafa Vincent Nzamwita, amesema mazungumzo yameanza kati ya Shirikisho la soka nchini humo na lile la Ujerumani kumtafuta kocha mpya.
Hatua hii inakuja baada ya kocha Johnny McKinstry raia wa Ireland Kaskazini kufutwa kazi mwezi uliopita baada ya matokeo mabaya ya kufuzu kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon na nafasi yake kuchukuliwa na Gilbert Kanyankore na Eric Nshimiyimana, ambao walifutwa kazi siku nne baada ya kupewa kibarua hicho.
Aidha, FERWAFA imesema Kaimu kocha Jimmy Mulisa na Naibu wake Vincent Mashami waliiongoza Amavubi Stars dhidi ya Ghana katika mchuano wa mwisho wa kufuzu kwa michuano ya AFCON, na kutoka sare ya bao 1-1 mwishoni mwa juma lililopita, hawataendelea kuifunza timu hiyo.
Rwanda imekuwa na mtindo wa kuwaajiri kwa muda mrefu:
Otto Pfister (1972-76), Rudi Gutendorf (1999).
Tangu mwaka 2001 Amvaubi Stars wamekuwa na makocha 10 na wengine watano wa mpito.
Ratomir Dujkovic (2001-04), Roger Palmegren (2004-06), Micheal Nees (2006-07), Josip Kuze (2007-08), Raoul Shungu (2008), Branko Tucak (2008-09).
Wengine ni pamoja na: Eric Nshimiyimana (2009-10), Sellas Tetteh (2010-11), Milutin ‘Micho’ Sredojević (2011-13), Eric Nshimiyimana (2013-14), Stephen Constantine (2014-2015), Lee Johnson (2015), Johnny McKinstry (2015-16), Gilbert Kanyankore (2016) na Jimmy Mulisa (2016).