-
by
Victor Abuso
Siku ya Jumatatu, kutakuwa na hafla ya kumtuza mchezaji bora wa mchezo wa soka duniani alimaarufu kama FIFA Ballon d’Or kwa mwaka wa 2015.
Hafla hiyo itafanyika jijini Zurich nchini Uswizi, jiji ambalo pia ni Makao makuu ya Shirikisho la soka duniani FIFA.
Wachezaji watatu wanaowania taji hili ni Lionel Messi raia wa Argentina anayeichezea klabu ya Barcelona nchini Uhispania pamoja na mchezaji mwezake Neymar ambaye anatokea nchini Brazil.
Mshindi wa mwaka 2014 Christian Ronaldo raia wa Ureno yupo kwenye orodha ya kutetea taji hili.
Lionel Messi ameshinda taji hili mara nne mfululizo mwaka 2009, 2010, 2011 na 2012 na sasa anasaka taji la tano.
Christiano Ronaldo naye ameshinda mara mbili mfululizo mwaka 2013 na 2014 na pia aliwahi kushinda mwaka 2008 naye anatafuta taji la ne.
Msimu uliopita, Messi aliifungia klabu yake mabao 58, na kuisadia Barcelona kunyakua ubingwa wa klabu bora duniani michuano iliyofanyika mwezi Desemba mwaka jana nchini Japan.
Ronaldo naye alitikisa nyavu mara 61 na Neymar akifunga mabao 39 alizocheza msimu uliopita.
Wanaowania tuzo ya kocha bora wa mwaka ni Luis Enrique raia wa Uhispania ambaye ni kocha wa Barcelona, Pep Guardiola pia raia wa Uhispania na kocha wa Bayern Munich nchini Ujerumani.
Mwingine ni Jorge Sampaoli raia wa Argentina ambaye ni kocha wa timu ya taifa ya Chile aliisadia kunyakua taji la Copa America mwaka jana.
Wanaowania taji la mwanadada au mwanamke bora katika mchezo huu wa soka ni pamoja na mchezaji wa timu ya taifa ya Marekani na klabu ya Houston Dash, Celic Sasic kutoka Ujerumani na Aya Miyama kutoka Japan.
CAF Confederation Cup
Simba snatch late winner against CS Sfaxien as Enyimba beaten
CAF Champions League
Sundown CL campaign has a pulse after beating Raja
CAF Champions League
TP Mazembe win CAF Women’s Champions league trophy
CAF Champions League
Mamelodi Sundowns Off to a Lukewarm Start in 2024/25 CAF Champions League
CAF Champions League
AL Ahly start CAF CL campaign with win over Stade d’Abidjan
CAF Confederation Cup
Simba make good start beating Bravos do Maquis
CAF Confederation Cup
Enyimba fall to Al Masry in Alexandria
CAF Confederation Cup
Zamalek got their Group D campaign off to a comfortable star
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...