-
-
by
Victor Abuso
Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA aliyesimamishwa kazi Sepp Blatter na Naibu wake Michel Platini huenda wakafungiwa kushiriki katika maswala ya soka kwa muda wa miaka saba ikiwa watapatikana na makosa ya kuhusika na ufisadi.
Ripoti inasema Kamati ya nidhamu ya FIFA huenda ikapendekeza adhabu hiyo baada ya ikiwa itabainika kuwa Blatter alitoa malipo yasiyokuwa rasmi kwa Platini yanayokadiriwa kuwa Dola Milioni 2.
Kamati hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi wake mwezi ujao wa Desemba, na imewafungia wawili hao kutoshiriki kwa shughuli za soka kwa siku tisini.
Platini na Blatter wote kwa pamoja wameendelea kukanusha kuhusika na tuhma hizo za ufisadi, huku Platini ambaye pia ni rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya akisema malipo aliyopata yalikuwa ni baada ya kumshauri Blatter kuhusu maswala mbalimbali ya soka.
Jaji Hans Joachim Eckert kutoka Ujerumani anaongoza uchunbguzi dhidi ya wawili hao.
Katika hatua nyingine, Blatter amesema alikuwa anahofia kufariki dunia siku chache zilizopita alipolazwa hospitalini baada ya kusumbuliwa na msongo wa mawazo.
Blatter mwenye umri wa miaka 79 alisema, “ Nilikuwa katikati ya Malaika na shetani aliyekuwa anawasha moto lakini Malaika walikuwa wanaimba nyimbo,”.
“Nilikaribia kufa.Wakati mwingine nilihisi mwili wangu umechoka na umefika mwisho,”. aliongeza Blatter.



Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe

Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...