-
-
by
Victor Abuso
Sepp Blatter rais wa zamani wa Shirikisho la soka duniani FIFA, pamoja na naibu wake Mitchel Platini na rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA wamepigwa marufuku ya kutoshiriki katika maswala ya soka kwa miaka minane.
Hatua hii imechukuliwa na Majaji wa Jopo maalum lililokuwa linachunguza tuhma za ufisadi dhidi ya wawili hao na siku ya Jumatatu, na limefikia maamuzi kuwa Blatter na Platini walihusika na ufisadi.
Blatter amekuwa akituhumiwa kumlipa Platini Dola za Marekani Milioni 2 malipo ambayo hayakufanywa kwa njia sahihi kwa mujibu wa kamati ya maadili ya FIFA.
Pamoja na adhabu hiyo, Blatter ambaye amekuwa akiongoza FIFA tangu mwaka 1998 alitozwa faini ya Dola 50,000 huku Platini akitozwa Dola 80,000.
Blatter na Platini wameendelea kusisitiza kuwa malipo hayo yaliyofanyika mwaka 2011 yalikuwa makubaliano ya watu wawili, baada ya Platini kufanya kazi ya kumshauri Blatter kuhusu maswala mbalimbali ya soka.
Majaji wa jopo hilo, wamepata wawili hao pia kwa hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na hatua hii inaamanisha kuwa Blatter mwenye umri wa miaka 79, huu ndio mwisho wake kujihusisha na maswala ya soka.
Platini mwenye umri wa miaka 60 ndoto yake ya kuchukua nafasi ya Blatter imedidimia kuelekea uchaguzi utakaofanyika mwezi Februari mwaka ujao.
Wawili hao wanaweza kukataa rufaa katika Mahakama ya Kimataifa ya Michezo kupinga adhabu ya jopo hilo.



Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe

Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...