Mali na Nigeria zitachuana jumapili hii katika fainali ya kuwania kombe la dunia katika mchezo wa soka baina ya wachezaji wasiozidi miaka 17.
Michuano hiyo imekuwa ikifanyika nchini Chile tangu tarehe 17 mwezi uliopita wa Oktoba na bara la Afrika limeweka historia kwa kufika katika hatua ya fainali hatua ambayo imepongezwa na rais wa muda wa Shirikisho la soka duniani FIFA Isaa Hayatoue.
Mali ilitinga katika hatua hiyo baada ya kuifunga Ubelgiji mabao 3 kwa 1 huku mabingwa watetezi Nigeria wakiwafunga Mexico mabao 4 kwa 2 katika michuano ya nusu fainali iliyochezwa siku ya Alhamisi.
Mataifa 24 kutoka mabara 6 yamekuwa yakishiriki katika mashindano ya mwaka huu na mbali na Nigeria na Mali zinazocheza fainali, Guinea na Afrika Kusini pia kutoka barani Afrika yalishiriki.
Hadi sasa mfungaji bora ni Victor Osimhem kutoka Nigeria ambaye ametikisa nyavu mara 9.
Michuano ya kwanza baina ya vijana chipukizi wasiodizi miaka 17 ilianza mwaka 1985 nchini China.
Nigeria kutoka barani Afrika ndio nchi iliyofanikiwa zaidi katika michuano hii kwa kushinda mataji 4 ikifuatwa na Brazil iliyonyakua mataji 3.
Ghana na Mexico zimeshinda mara mbili na fainali ya mwaka 2017 itachezwa nchini India.