-
-
by
Victor Abuso
Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA aliyesimamishwa kazi kwa siku 90 kwa tuhma za ufisadi Sepp Baltter amefika mbele ya Majaji wa Kamati ya maadili ya Shirikisho hilo jijini Zurich nchini Uswizi.
Blatter ambaye aliambatana na wakili wake hakuwaambia wanahabari lolote wakati akiingia katika chumba cha mahojiano.
Kabla ya kuhojiwa na Kamati hiyo, Blatter aliyaandikia barua mashirikisho yote ya soka duniani kukosa imani na wajumbe wa Kamati hiyo ya maadili.
Blatter mwenye umri wa miaka 79 amekuwa akikanusha madai ya kuhusika na tuhma za rushwa katika Shirikisho hilo aliloliongoza tangu mwaka 1998.
Pamoja na Blatter, Mitchel Platini rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya anayetuhumiwa kulipwa Dola Milioni 2 na Blatter amesema hatofika mbele ya kamati hiyo siku ya Ijumaa badala yake atamtuma wakili wake.
Wawili hao wamekanusha kuhusika na tuhma za ufisadi na ikiwa watapatikana na kosa, huenda wakafungiwa kushiriki katika maswala ya soka kwa muda wa miaka saba.
Wakati hayo yakijiri, rais wa Urusi Vladimir Putin amesema Blatter anastahili kushinda tuzo ya amani ya Nobel kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akiifanya katika Shirikisho la la FIFA.
Urusi itakuwa mwenyeji wa kombe la dunia mwaka 2018 na rais Putin amekuwa akiyashtumu mataifa ya Magharibi kwa kumlenga Bwana Blatter kisiasa.



Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe

Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...