-
-
by
Victor Abuso
Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA kwa mara nyingine amesisitiza kuwa hatajiuzulu kabla ya tarehe 26 mwezi Februari mwaka ujao wakati uchaguzi mwingine utakapofanyika.
“Nitaacha tu kufanya kazi tarehe 26, sio kabla ya siku hiyo,” Blatter ameliambia Jarida la Ujerumani Bunte.
“Nitapambana hadi tarehe 26.Kwa binafsi yangu.Na kwa FIFA.”
Blatter amekuwa akikabiliwa na shinikizo za kujiuzulu kutokana na tuhma za ufisadi ambazo anakanusha kuhusika.
Aidha, amesisitiza kuwa hana hofu kuhusu uchunguzi unaofanywa na viongozi wa mashtaka nchini Uswizi .
“Huu ni uchunguzi tu wa kawaida. Sijafunguliwa mashtaka. Sitashirikiana na maafisa hao,” Blatter mwenye umri wa miaka 79 amesisitiza.
Wiki iliyopita, wafadhili wa FIFA Coca-Cola, McDonald’s, Visa na Budweiser walimtaka Blatter ajiuzulu kwa kile walichokisema mabadiliko yanaweza kufanyika tu ikiwa ataondoka.
Hata hivyo, Blatter amesema kuwa wafadhili wengine wa kutengeza jezi Adidas, Hyundai na Gazprom kutoka Urusi wamesimama naye na wanamuunga mkono.
Mbali na Blatter, rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Mitchel Platini amesisitiza kuwa hana cha kuficha kuhusu Dola Milioni 2 alizolipwa na FIFA.
Viongozi wa mashtaka nchini Uswizi wanasema alipokea fedha hizo kwa njia zisizoeleweka na kumtuhumu kuhusika na ufisadi.
Kamati ya nidhamu inakutana kuwajadili Sepp Blatter na Mitchel Platini.



Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe

Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...